KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, January 6, 2011

Wala-Watu wa Tsavo walikuwa Simba wawili



Wala-Watu wa Tsavo katika maonyesho ya Uwanjani katika Musiamu ya Historia ya Kimaumbile jijini Chicago, Illinois.Wala-Watu wa Tsavo walikuwa Simba wawili waliojulikana sana kwa kuwala binadamu. Simba hawa walisababisha vifo vya idadi kubwa ya wajenzi wa Reli ya Kenya-Uganda, tangu Disemba, 1898


Historia





Mnamo Machi 1898, wakati wa ujenzi wa Reli ya Kenya-Uganda, mhandisi John Henry Patterson aliongoza ujenzi wa daraja juu ya Mto Tsavo nchini Kenya. Wakati wa ujenzi huu, wafanyikazi wengi wa India waliuawa na simba wawili wa kiume (Simba wa Tsavo), ambao walivamia watu hemani mwao na kuwararua. Wajenzi hawa walijenga maboma yenye kuta za miiba kuzunguka hema zao ili kuwaepuka wala-watu hawa; lakini simba hawa waliweza kujipenyeza. Patterson alijaribu mara kadhaa kuwawekea mitego na kuwafukuza usiku kutika mtini. Baaada ya majaribio mengi bila mafanikio, hatimaye alimpiga risasi mmoja wao mnamo Disemba 9, 1898. Wiki tatu baadaye, mnyama wa pili alipatikana na kuuawa. Idadi kamili ya watu waliouawa na wanyama hawa haijadhihirika. Wakati wa uhai wake, Patterson alitoa takwimu nyingi tofauti tofauti, moja ikikisia kwamba kulikuwa na waadhiriwa wengi, takribani 135.[1][2] Utafiti wa hivi maajuzi unaonyesha kwamba takwimu hizi zilikuwa takribani 35.

Patterson anaandika kuwa alimjeruhi simba wa kwanza akitumia risasi kutoka bunduki aina ya martini-Enfield .303. Risasi hii ilimpata katika miguu ya nyuma na akafanikiwa kutoroka. alirudi usiku akijaribu kumsaka Patterson hata alipojaribu kumwinda. patterson alimpiga risasi mara kadhaa akitumia bunduki ya .303 Lee Enfield, huku akimfuatilia keshoye na kumpata akiwa amefariki. Kwa ujumla, alimpiga risasi mara tano. Simba wa pili alipigwa risasi mara tano kwa kutumia bunduki ya .303 Lee Enfield, lakini bado aliweza kusimama na kujaribu kumsogelea kwa maumivu makali, ambapo alimpiga risasi mbili zaidi, moja katika kifua na ya pili kwa kichwa na akamuua. Anadai kuwa simba huyo alifariki huku akining'ini katika taga la mti lililoanguka, bado akijaribu kumfikia Patterson.

Baada ya kutumika kwa miongo miwili na nusu kama matandiko ya Patterson, ngozi za simba hao ziliuzwa kwa Musiamu ya Uwanjani ya Chicago kwa jumla ya Dola za Marekani 5,000. Simba hao walifika kwa Musiamu katika hali mbaya. Walijengwa upya na sasa hivi wako katika maonyeshho ya kudumu pamoja na viwiliwili vyao. Simba waliopandikwa hapo wako na kipimo kidogo kuliko unene wa kutisha ambao Patterson anausimulia, pengine kwa kuwa Patterson alidanganya juu ya unene huo, au kwa sababu walikuwa wamepunguzwa ili kutumika kama matandiko ya Kombe nyumbani mwa Patterson.

Masimulizi ya Patterson yalichapishwa katika kitabu chake cha 1907, The Man-Eaters of Tsavo.

Utafiti wa Kisasa



Sampuli za wanyama hawa wawili katika Musiamu ya Chicago wanajulikana kama FMNH 23970 (aliyeuawa Disemba 9) na FMNH 23969 (aliyeuawa Disemba 29). utafiti wa hivi maajuzi umefanya kutokana na uchambuzi wa sahii ya Kiisotopia (Isotopic Signature) mabadiliko ya Carbon-13 (Δ13C) na Nitrogen-15 katika collagen ya mifupa yao na keratin katika nywele yao. Kwa kutumia makisio kuwa binadamu walioasiriwa walikuwa na kilo 20 za nyama ya kulika pamoja na hati tofauti za kiisotopia (Isotopic Signatures) za nyama ya binadamu ikilinganishwa na windo la kawaida la simba, uchambuzi huu unakisia kuwa FMNH 23969 alikula kiwango cha watu 10.5 na FMNH 23970 akala kiwango cha binadamu 24.5.[4] Takwimu hizi zinatoa idadi ya waasiriwa 35 ambayo Patterson alikuwa amedai kuwa 135..[5]

Vyanzo Vilivyokisiwa Kuchangia Ulaji wa Binadamu

Madhanio mbalimbali kuhusu tabia ya ulaji watu yamepitiwa na Kerbis Peterhans na Gnoske (2001) na Patterson (2004). majadiliano yao yanajumuisha yafuatayo:

Kuzuka kwa maradhi ya Nagana mnamo 1898 yalipunguza windo la kawaida la simba, wakilazimishwa kutafuta pato jingine la chakula.
Simba wa Tsavo wanaweza kuwa walizoea kuwapata watu waliokufa wakivuka Mto Tsavo. Wafanyi biashara ya kuuuza watumwa waliojikita Uunguja walikuwa wakivuka mto huo mara kwa mara.
mila ya Wajenzi wa reli wa dini ya Hindu ya kuwatupa wafu baada ya kuwachoma ilipelekea simba hao kuwala wafu hao.
Madai mengine ni kuwa simba wa kwanza alikuwa na jino lililoumia sana na hili linaweza kuwa lilikandamiza uwezo wake wa kutafuta windo la kawaida, kwa hivyo akawageukia binadamu. Ushahidi kuhusu madai haya umeonyeshwa katika karatasi zilizopitiwa kwa undani na Neiburger na Patterson (2000, 2001, 2002)na pia katika kitabu cha Bruce Patterson (2004)

Utamaduni Uliofana




Kitabu cha Patterson kilitumiwa kama msingi wa filamu Bwana Devil (1952) na The Ghost and the Darkness (1996) ("The Ghost" na "The Darkness" ni majina waliyopewa Simba hawa wawili wala-watu)

No comments:

Post a Comment