KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Wake wenza watwangana msibani


WANAWAKE wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamejikuta wakishindwa uvumilivu na kuanza kutupiana maneneo na hatimaye kushikana na kuoneshana adabu katika msiba wa shemeji yao huko Morogoro vijijini eneo la Kisaki.
Wanawake hao wamejikuta wakitwangana makonde hadharani baada ya kujigundua kuwa wake wenza katika msiba huo.

Wanawake hao warembo walifika msibani hapo kwa nyakati tofauti huku mmoja wao akiwa ameongozana na baadhi ya wanandugu kwa basi lililobeba wafiwa na mmoja akiwa amekuja mwenyewe baada ya kuchelewa basi lililobeba wafika kwenda kuzika.

Wanawake hao kila mmoja akiwa amefika msibani hapo katika msiba wa shemeji yake ambapo mpenzi wao alikuwa amefiwa na kaka yake.

Bila kujifahamu wakiwa katika msiba huo walishughulika na shughuli za msibani hapo huku kila mmoja akiwa na ufahamu alikuwa ukweni na kuonyesha nidhamu ya hali ya juu msibani hapo.

Hata hivyo kijana aliyekutanisha wanawake hao aliyetambulika kwa jina la Adamu[30] mkazi wa Sinza Mori mfanyakazi wa shirika la Umeme alikuia katika wakati mgumu baada ya kutokuwa huru kutokana na hali hiyo kwa kuwa hakutarajia kama wote wangehudhuria msiba huo.

Katika hali ambayo haijategemewa, dada wawili wa Adamu walianza kunong’ona kuhusiana na tabia chafu ya kaka yao huyo kuwakutanisha wanawake hao na wakati wanazungumza mmoja wao alisikia mazungumzo hayo wakati dada hao wakionyeshana wanawake hao ambapo mmoja alikuwa akifahamika na wengi na mwingine alikuwa akifahamika na wachache.

Mwanamke huyo mmoja aliyesikia mazungumzo hayo alimfata mchumba wake huyo na kumuuliza Adamu alikana kumtambua kama mchumba wake na alimjibu na kudai walikuwa wakifanyabiashara pamoja

Hata hivyo mwanamke huyo alitaka ahakikishe hilo na alimfata mwanamke mwenzake na kumuuliza yuko katika msiba huyo kama nani na alimbainishia kuwa Adam ni mchumba wake na baadhi ya ndugu walikuwa wakimfahamu.

Mara baada ya kupata jibu hilo varangati likaanza mahali hapo na kuanza kurushiana maneno ya hapa na pale hadi ikapelekea amani kutoweka eneo hilo na kupelekea kutwangana makofi na hatimaye kushikana na kuoneshana adabu ya ukweli ukweli huku kila mmoja akijinadi kuwa ni mchumba wa Adam.

Hata hivyo baadhi ya ndugu waliwasihi wanawake hao kuacha ugomvi lakini walikuwa katika wakati mgumu na mmoja wao aliondoka na gari lililowabeba wanandugu na kurudi jijini Dar Es Salaam huku mmoja alikuwa akisubiri jibu kamili kutoka kwa Adam kama alikuwa mchumba feki ama la.


Hata hivyo mara baada ya tatu kuisha katika msiba huo, wanandugu walimkalisha chini Adamu ili aweze kubainisha alikuwa akimuhitaji mwanamke yuopi kati ya wale ili aweze kuoa na kumkanya tabia aliyoionyesha pale msibani na kuweka doa msiba.

Hata hivyo jibu alilolitoa Adamu halikupendezwa na wanandugu hao kwani aliweza kuwajibu alikuwa bado hajafahamu yupi aweze kumuoa kwani alikuwa akiwachunguza na kubainisha angemuoa mmoja wao kwan I alionekana kuwa na tabia ambazo zinaridhisha.

“Nitawajulisha baada ya kufika Dar es salaam, na nitaanza kufata hatua za kuoa mara baada ya msiba huu kuisha, naomba mnisamehe" alifafanua Adamu

No comments:

Post a Comment