KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, January 11, 2011

Ubungo yafurika wengi wasitisha safari


Jana watu wakiwa wamefurika katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani wakihangaika na usafiri wa kurudi mikoani baada ya stendi hiyo kufurika kupita kiasi na kusababisha usafiri kuwa mgumu.
Ilibainika kuwa jana watu wengi walikuwa wakihitaji usafiri wa kurudi mikoani kutokana na kuwa muda wa likizo kwa wanafunzi ulikuwa umeisha na wafanyakazi wengi walimaliza likizo zao za mwishoni mwa mwaka.

Hali hiyo iliacha wasafiri hao wakihaha kusaka usafiri wa kuwarudisha mikoani kwa kuwa mabasi yote yalikuwa yamejaa.

Mabasi mengi yamekuwa yakionekana kupata tenda maalumu za mashule kurudisha wanafunzi mikoani na kusababisha ukosefu wa usafiri na abiria walioweza kusafiri walidai kuwa waliweka oda maalumu wiki moja kabla.

Baadhi ya abiria walioweza kuzungumza na Nifahamishe.com walisema “usafiri ni shida mno kama unavyoona, tumekuja hapa toka saa 12 asubuhi na sasa inaenda saa 7 hatujapata usafiri, inabidi tuahirishe maana hamna dalili ya usafiri”.

Huyo alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wakihitaji usafiri wa kuelekea mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment