KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, January 29, 2011

Serikali yakiri bodi ya mikopo elimu ya juu ni tatizo


SERIKALI imekiri kuwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu inachangia matatizo ya migomo vyuoni wka kuwa bodi hiyo imekwua na utendaji mbovu.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa wakati alipokuwa akihojiwa na Television ya Taifa TBC 1.
Alisema bodi hiyo ni sababu ya kuchangia migogoro vyuoni kwa kuwa imekuwa haishirikiani vyema na taasisi zingine husika zinazohusiana na kutatua matatizo hayo.

Alisema Wizara ya Elimu imebaini bodi hiyo kuhusika moja kwa moja kwa migogoro vyuoni kutokana mna utendaji wake ambao hautoshelezi.

Hata hivyo amewataka wanafuzni kuwa watulivu wakati kipindi hiki wanashughulikia matatizo na kurekebisha utendaji wa bodi hiyo

No comments:

Post a Comment