KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Mhasibu Tanesco Kortini


MHASIBU MWANDAMIZI wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) Lilian Chengula amepandishwa kortini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shitaka la kujinyakulia shilingi bilioni 1.3 za shirika hilo.


Mshitakiwa huyo alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mustapha Siani huku upande wa Mashitaka uliongozwa na waendesha Mashitaka watatu.

Chengula amekabiliwa na kusomewa mashitaka yapatayo 85 yakiwemop ya kuhujumu uchumi na ya wizi kutoka ndani ya shirika la umeme Tanzania.

Hati ya mashitaka ilionyesha kuwa, alitenda makosa hayo kati ya mwaka 2009 hadi Septemba 2010 katika ofisi za shirika hilo wilayani Kinondoni.


Imedaiwa kusababisha hasara ya Sh. bilioni 1.3 kinyume cha Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Hata hivyo jana mshitakiwa huyo hakuweza kupatiwa dhamana kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kati ya shitaka aliloshitakwia nalo mahakamani hapo na kusubiri amri kutoka kwa DPP.

Mahakama itatoa uamuzi leo juu ya dhamana ya mshitakiwa huyo

No comments:

Post a Comment