KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Maambukizi mapya HIV yapungua Zimbabwe

Uchunguzi kuhusu virusi vya HIV nchini Zimbabwe umeonesha mabadiliko makubwa ya tabia za ngono kwa wanaume, yamesaidia kupungua kwa watu wazima wenye virusi vya HIV vinavyosababisha maradhi ya Ukimwi

Mapambano dhidi ya Ukimwi yapungua Zimbabwe


Idadi ya watu wenye virusi vya HIV imeshuka hasi asilimia kumi na sita mwaka 2007, kutoka asilimia ishirini na tisa miaka kumi iliyopita.

Uchunguzi huo umeonesha uzoefu wa mtu mmoja mmoja kushuhudia kifo cha mtu aliyekufa kwa UKIMWI, kumeongeza woga wa wa kuambukizwa na pia imeimarisha kampeni za kuwataka watu kuwa na uhusiano na mpenzi mmoja mwaminifu kama kampeni zinavyoelezwa na vyombo vya habari, makanisa na sehemu za kazi.

Uchunguzi huo vilevile umebainisha uchumi mbovu wa Zimbabwe umesaidia kubadilisha tabia za watu , kwa sababu wanaume hawana pesa nyingi za kuhonga

No comments:

Post a Comment