KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, January 29, 2011

Jela miaka 10 ukibainika kuambukiza virusi makusudi


ATAKAYEBAINIKA kuambuikiza na kusambaza virusi vya ukimwi kwa makusudi atatumikia kifungo cha miaka 10 jela.
Hayo yamebainishwa jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Bi. Celina Kombani alipokuwa akijibu swali Bungeni.

Kombani amebainisha kuwa, mtu yeyote akibainika anasambaza virusi vya ukimwi kwa makusudi atapewa adhabu ya kifungo cha miaka mitano hadi kumi kutokana na kosa hilo.

Amesema kusambaza virusi hivyo kwa makusudi kwa watu wengine ni kosa la jinai kisheria

No comments:

Post a Comment