KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Hague azuru Tunisia baada ya maandamanoMaandamano nchini Tunisia
Waziri wa mashauri ya nchi za Kigeni wa Uingereza, William Hague, yuko nchini Tunisia katika siku ya kwanza ya ziara yake katika mataifa yaliyokumbwa na vuguvugu la maandamano ya wananchi wanaoshinikiza kufanyika mageuzi ya kisiasa.

Bwana Hague atakutana na mawaziri wa ngazi ya juu katika serikali ya Tunisia, na kuwaambia kuwa Uingereza iko tayari kuwapa msaada katika utekelezaji wa mageuzi yenye manufaa.


Huku kimbunga cha mabadiliko kinapozidi kuvuma Kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati William Hague atatumia siku tatu zijazokuzuru mataifa matano.


Bwana Hague
Anaanzia ziara yake katika chanzo cha maandamano Kaskazini mwa Afrika - Tunisia - ambako Rais Ben Ali alitimuliwa madarakani mwezi uliopita.

Ujumbe wake kwa mataifa yote anayozuru ni kuwa Serikali ya Uingereza iko tayari kutoa msaada wa hali na mali kuhakikisha kuwa mabadiliko ya kisiasa ya amani yanatakelezwa, na wakati huohuo kusaidia kujenga taasisi za kidemokrasia katika mataifa hayo.

Uingereza inashirikiana na mataifa mengine ya Magharibi kufuatia wasiwasi kwamba ghasia na misukosuko katika mataifa ya Afika Kaskazini, yanahatarisha usalama katika eneo lote na kwamba mabadiliko bora yanapaswa kufanywa.

No comments:

Post a Comment