KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Gates atarajia mahusiano mema na China



Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates.

Robert Gates na waziri mwenzake wa China Gen. Liang Guanglie baada ya mazungumzo na waandishi habari.
Maingiliano

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amesema anaamini uhusiano wa kijeshi kati ya nchi yake na jamhuri ya umma wa China utaimarika.Matamshi hayo ameyatoa baada ya mazungumzo pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Yang Jiechi hii leo.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates aliyeko ziarani katika jamhuri ya umma wa China tangu jumapili iliyopita amepangiwa kukutana baadae leo mchana na rais Hu Jintao katika wakati ambapo nchi hizi mbili zinajitahidi kumaliza mivutano yao katika sekta ya kijeshi.

"Nnaamini maendeleo ya muda mrefu katika uhusiano kati ya majeshi ya nchi zetu" alisema waziri wa ulinzi Robert Gates,mbele ya waandishi habari, mwanzoni mwa mazungumzo yake pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa jamhuri ya umma wa China,Yang Jiechi.

"Tunaamini ziara ya rais Hu Jintao wiki ijayo itachangia pakubwa katika kuimarisha uhusiano kati ya China na Marekani" ameongeza kusema waziri wa ulinzi wa Marekani.

Rais Hu Jintao amepanga kuitembelea Marekani kuanzia january 18 hadi 21 ijayo.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Yang Jiechi amesema ziara ya waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates ni "ushahidi wa umuhimu unaotolewa na China kwa uhusiano kati ya nchi zao mbili na pia katika uhusiano wa kijeshi wa madola haya mawili makuu.

Mwaka jana China ilifutilia mbali ziara ya waziri Gates,baada ya kusitisha kwa ghafla maingiliano ya kijeshi baada ya Washington kutiliana saini pamoja na Taiwan mkataba wa biashara ya silaha wenye thamani ya zaidi ya dala bilioni sita.

Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Robert Gates na waziri mwenzake wa China Gen. Liang Guanglie baada ya mazungumzo na waandishi habari.
Maingiliano yameanza upya december mwaka jana kufuatia ziara ya ujumbe wa kijeshi wa China nchini Marekani.

Hata hivyo mazungumzo aliyokuwa nayo waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates mjini Beijing hayakusaidia pakubwa.Jana waziri Gates alizungumzia umuhimu wa kuanzishwa majadiliano ya kimkakati na namna ya kuupanua ushirikiano akisema:

"Miongoni mwa mada ni pamoja na kuimarisha usalama baharini,kukabiliana na changamoto za kuenezwa silaha za kinuklea,teknolojia ya anga za juu,na makombora,kuendeleza amani na usalama katika raas ya Korea kwa kuzihimiza pande hizo mbili ziwajibike na kuitakasa raas ya Korea ya silaha za kinuklea."

Waziri wa ulinzi wa China jenerali Liang Guanglie hakutaka kusema chochote kuhusu pendekezo hilo

No comments:

Post a Comment