KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Wabunge Chadema wasusia kikao tena


JANA Bunge la 10 limeanza kikao chake na bunge hilo limeonekana kuanza kwa moto baada ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] kususia kikao hicho na kutoka nje ya ukumbi wa bunge.
Wabunge hao walichukua umamuzi huo baada ya kupinga mabadiliko ya kanuni za bunge yaliyowasilishwa bungeni humo jana.

Katibu wa Bunge, Job Ndugai jana aliwasilisha hoja ya kufafanua tafsiri sahihi ya kambi halali ya upinzani bungeni na baadae kuachia wabunge kupitisha hoja hiyo bungeni.

Kambi ya upinzani ilitakiwa kuwa moja kwa kuungana kwa vyama vyote vya upinzani na kupatikana kwa kambi hiyo bungeni kutokana na kanuni za bunge na kuvunja kambai ya upinzani kuwa na wabunge zaidi ya asilimi 12.5kama ilivyotafsiriwa awali.

Katika hali isiyo ya kawaida wabunge wa chama hicho hawakukubaliana na hoja hiyo iliyowasilishwa bungeni hapo na punde wabunge hao wakasusia kikao hicho na kutoka nje ya ukumbi wa bunge.

Wabunge hao walipingana na hoja hiyo na kutokubali kuungana na vyama vingine vya upinzani wakiwemo CUF, NCCR, TLP na vinginevyo na kutaka kuwepo kwa kambi zaidi ya moja.

Akipinga hoja hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Chadema, Freeman Mbowe alisema “ hatutaki kuungana na vyama vingine, tusilazimishwe ndoa ya lazima bila kuridhika” nitahakikihsa nitatafuta haki yetu hadi ipatikane.

Wabunge hao walikiita chama cha CUf kuwa kigegeuge na kukiiita CCM ‘B’ kwa kukiona chama hicho kinakubaliana na matakwa ya chama cha Mapinduzi

Awali katika bunge lililopita chama hicho vilijipa vyeo mbamimbali vya kuongaza kambi ya upinzani bungeni bila ya makubaliano na vyama vingine

No comments:

Post a Comment