KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Waangua kilio katika ofisi ya intaneti Café


WASICHANA wawili waliomaliza katika shule ya sekondari Mtinko mkoani Singida wamejikuta wakiangua kilio mara baada ya kuona matokeo yao katika ofisi hiyo.
Wasichana hao walifika katika ofisi hiyo jana majira ya jioni na kuomba msaada ya kuangaliziwa matokeo yao ya kidato cha nne.

Wakati wakiangaliziwa matokeo hayo huku wakiwa na shauku ya kufahamu matokeo hayo, ndipo walipofanikiwa kuona majina yao na alama zao walizopata na ndipo ghafla kelele za mayowe zilisikika katika chumba hicho na kuwaacha wateja wengine waliokuwa katika chumba hicho kushutuka kutokana na mayowe hayo.

Mara baada ya mayowe hayo binti mmoja alianza kulia kwa kugundua kufeli mitihani hiyo na kuambulia failed yenye alama ya pointi 35 na mwingine nae alimuunga mkono mwenzake kwa kuangulia kilio kwa kugundua kupata division foo ya 31.

Hata hivyo wasichana hao waliweza kupewa ushauri kidogo na watu waliokuwa mahali hapo na kutakiwa kujipanga upya kurudia mitihani hiyo kwa kuweka juhudi zaidi.

Hata hivyo mabinti hao waliweza kuiambia nifahamishe kuwa walifeli mitihani hiyo kwa kuwa walikuwa walikuwa wanakabilia na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kutomaliza silabasi, upungufu wa walimu na nyingine nyingi walizoorodhesha kutoka vinywani mwao.

Matokeo ya mwaka huu yanaonyesha nusu ya watahiniwa wamefeli mitihani hiyo iliyofanyika Oktoba mwaka jana nchini kote

No comments:

Post a Comment