KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Ushauri wa Jinsi ya Kulima Bangi


Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amekuwa mkulima wa bangi mwenye mafanikio ziro baada ya kupiga simu polisi akiwafahamisha kuwa ameanza kulima bangi akitaka kujua adhabu zitolewazo kwa kulima angalau mmea mmoja wa bangi.
Robert Michelson, 21, alipiga simu polisi na kuwauliza adhabu ambayo anaweza kupewa iwapo atakamatwa akilima mmea mmoja wa bangi.

Polisi kwa kutumia namba ya simu aliyoitumia, waliweza kuigundua nyumba yake ambapo msako wa polisi ulifanikiwa kugundua mimea michache ya bangi.

Michelson alitiwa mbaroni kwa kumiliki mimea hiyo kinyume cha sheria na aliachiwa huru kwa dhamana ya dola 5000

No comments:

Post a Comment