KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 2, 2010

Mcheza Soka Akatwa Vipande Vipande Kwa Kupora Demu wa Mtu


Mcheza soka wa kimataifa wa nchini Guatemala ameuliwa na mwili wake kukatwa vipande vipande na kuwekwa kwenye mifuko mitano ya plastiki.
Polisi nchini Guatemala wameupata mwili wa mchezaji soka wa kimataifa wa nchini humo, Carlos Mercedes Vasquez ukiwa umekatwa vipande vipande na kuwekwa kwenye mifuko mitano ya rambo.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa Carlos Mercedes Vasquez ambaye alikuwa kiichezea timu ya Malacateco ya ligi daraja la kwanza nchini humo aliuliwa na mwili wake kukatwa vipande vipande.

Msemaji wa polisi wa Guatemala alisema kuwa mwili wa Vasquez ulipatikana siku ya jumapili ukiwa umeambatanishwa na ujumbe unaosema "Umeuliwa kwa kutembea na wanawake wa watu".

Vasquez mwenye umri wa miaka 27, alitekwa siku ya jumamosi wakati alipokuwa pamoja na marafiki zake akiendesha gari kuelekea mjini.

Mwili wake ulipatikana jumapili kwenye kitongoji cha Malcatan nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo.

Polisi nchini Guatemala wameanzisha uchunguzi kujua sababu halisi ya kifo cha Vasquez

No comments:

Post a Comment