KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Marekani yamtaka Gbagbo kung'atuka



..Rais Gbagbo wa Ivory Coast
Marekani imemtaka rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, kukubali kuwa alishindwa katika uchaguzi wa hivi maajuzi na kumkabidhi madaraka mpinzani wake, Alassane Ouattara.

Afisa mmoja wa ikulu ya White House amesema rais Obama anamzingatia kuwa Bwana Ouattara ndiye aliyeshinda uchaguzi huo kihalali.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini,Thabo Mbeki, anatarajiwa kuwasilisha ripoti kwa umoja wa Afrika baada ya siku mbili za kujarbu kusuluhisha mgogoro huo nchini Ivory Coast.

Jumuiya ya kiuchumi kwa mataifa ya Afrika magaribi ECOWAS ambayo pia imemtangaza bwana Ouattara kuwa mshindi, inatarajiwa kuandaa mkutano maalum hivi leo Jumanne nchini Nigeria.

Jana Jumatatu, umoja wa mataifa ulisema unawaondoa japo kwa muda yapata wafanyikazi wake 500 wanaotoa huduma zisizokuwa za lazima kutoka nchini Ivory Coast kutokana na mzozo huo

No comments:

Post a Comment