KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Mafuriko Australia yasababisha uharibifu


Mafuriko Australia

Mafuriko nchini Australia yameenea hadi kusini mwa nchi hiyo na kusababisha hasara kubwa katika miji kadhaa jimbo la Victoria.

Mafuriko hayo yaliyovunja rekodi yanatishia mji wa Echucha, uliopo kwenye mpaka wa Victoria na Wales ya Kusini.

Mapema wiki hii maeneo kadhaa ya Brisbane yalifurika baada ya wiki kadhaa za mvua nyingi.

Maeneo mengi ya mashariki mwa Australia kutoka Queensland hadi Tasmania pia yamekumbwa na mafuriko.

Watoa huduma za dharura katika jimbo la Victoria wamesema athari iliyosababishwa kaskazini mwa jimbo hilo ni kubwa zaidi.

Katika mji wa Echuca wakaazi wamesema wamekuwa katika hali ya hofu huku mto wa Campaspe ukiendelea kufurika.

Baadhi ya familia zimetengwa na mafuriko hayo na athari kamili bado haijulikani.

Wiki iliyopita mafuriko katika jimbo la Queensland yaliwaua takriban watu 18 na wengine zaidi ya 12 hawajulikani waliko.

Sehemu kadhaa za Brisbane zilididimia na marekebisho yatachukua miezi kadhaa.

Watabiri wamesema kuwa mvua mkubwa huenda ikaendelea kunyesha hadi mwezi wa Machi

No comments:

Post a Comment