KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, December 30, 2010
JK aridhia katiba mpya
SAKATA la mchakato wa kupatikanfa katiba mpya umeleta matumaini kwa wananchi baada ya rais Jakaya Kikwete kuridhia na kuahidi kuunda tume maalum ya kupatikana katiba hiyo.
Rais Jakaya Kikwete aliyasema hayo katika salamu zake za mwaka mpya kwa wananchi kwa kulihutubia Taifa kwa njia ya Vyombo vya habari.
Rais Kikwete ameahidi kuunda tume maalum kutoka makundi tofauti ndani ya jamii ili kufanikisha mchakato a katiba hiyo ambayo inaonekana kuliumiza kichwa wadau mbalimbali nchini kutokana na tofauti zinazojitokeza.
Alisema Tume hiyo itaongozwa na mwanasheria aliyebobea katika masuala ya katiba, kushirikisha wananchi, vyama vya siasa, mashirika ya dini, wafanyabiashara, vikiwemo na vyama vya kiraia ili kutoa maoni kuhusu Katiba ya nchi.
Kufuatia ridhaa hiyo baadhi ya wadau na wananchi kwa ujumla wamempongeza Rais kwa kuonyehsa kuwa ni rais muelewa na anayekwenda na wakati kwa kuridhia kutengenezwa kwa katiba mpya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment