KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Bundesliga.Dortmund bingwa wa nusu msimuGroßansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Bastian Schweinsteiger wa Bayern Munich (kushoto) akipambana na Christoph Metzelder wa Schalke Katika ligi ya soka ya Ujerumani Bundesliga, Schalke 04 imeigaragaza Bayern Munich kwa mabao 2-0.

Borussia Möenchengladbach wameangukia pua baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Hannover.

Eintracht Frankfurt nayo ikaibuka mshindi dhidi ya Mainz kwa kuifunga mabao 2-1.

Katika mechi nyingine Freiburg iliishinda Sport Verein Hamburg bao 1-0, wakati Vfb Stuttgart na Hoffenheim zilitoshana nguvu pale zilipotoka suluhu ya bao 1-1 nazo Wolfsburg na Werder Bremen hakupatikana mbabe baada ya timu hizo kutoka sare bila kufungana.

Borussia Dortmund ambayo inamiadi leo Jumapili na 1FC Nuremberg imejipatia taji lisilo rasmi la ubingwa wa majira ya mapukutiko, kwa mara ya tatu katika historia ya club hiyo. Hadi sasa Borussia Dortmund imeshinda michezo 12 kati ya 14 msimu huu

No comments:

Post a Comment