KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

11 wafa katika kampeni Nigeria


Rais Goodluck Jonathan



Watu 11 wamekufa katika mkanyagano kwenye mkutano wa kisiasa nchini Nigeria.

Mkutano huo uliofanyika katika mji wa kusini wa Harcourt, ulikuwa sehemu ya mkutano wa kampeni wa rais Goodluck Jonathan, kabla ya uchaguzi wa mwezi April.

Uchunguzi

Watu wengine 29 wanasemekana kujeruhiwa katika mkutano huo, ambao ulifanyika kwenye uwanja wa michezo.

Rais Jonathan ameagiza kufanyika kwa uchunguzi na kusema tukio hilo lilikuwa "la kusikitisha, bahati mbaya na la kujutia," na kuongeza: "Naomboleza na wale wanaoomboleza."

Umati huo ulishituka, baada ya polisi kufyatua risasi hewani, kujaribu kutawanya watu katika milango ya kuingiliwa uwanjani, wakati watu wakitoka, kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo na kukaririwa na shirika la habari la Reuters.

"Kulikuwa na kundi kubwa la watu, na sehemu ilikuwa imejaa," amesema Ken Saro-Wiwa, msaidizi wa Rais Jonathan wa masuala ya kimataifa, ameiambia Reuters.

"Ni mwisho wa kusikitisha katika siku iliyoanza vizuri," amesema Bw Saro-Wiwa

No comments:

Post a Comment