KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 8, 2010

Wamuona Shetani , Wajirusha Toka Ghoro ya Pili


Mtoto mmoja mchanga amefariki dunia na watu 10 kujeruhiwa nchini Ufaransa baada ya kundi la watu kujirusha toka ghorofani wakidhani wamemuona shetani kumbe ni jirani yao aliyekuwa akirandaranda uchi usiku wa manane.
Mwanaume toka Angola aliyekuwa akitembea uchi wa mnyama usiku wa manane mjini Paris, Ufaransa amesababisha majirani zake wajirushe toka ghorofani wakidhani wamemuona shetani.

Tukio hilo lilitokea kwenye mji wa La Verriere magharibi mwa Ufaransa ambapo watu 10 walijeruhiwa na mtoto wa kike wa miaka miwili amefariki dunia baada ya kundi la watu kujirusha toka ghorofa ya pili.

Ilikuwa ni saa tisa usiku wakati mmoja wa watu 13 waliokuwa wakikaa ghorofa ya pili ya jengo moja mjini humo, aliposikia mtoto wake mchanga akilia.

Mwanaume huyo ambaye alikuwa uchi wa mnyama alinyanyuka kwenda kumuangalia mtoto wake ndipo alipokutana na wakazi wengine wa jengo hilo ambao walimhisi kuwa ni shetani.

Wakazi wa jengo hilo walimjeruhi mikononi mwanaume huyo kwa visu na kisha kumtupa nje ya jengo hilo kupitia mlangoni.

Mwanaume huyo alipolazimisha kuingia tena ndani, wakazi wa jengo hilo walimhisi kuwa yeye si mtu wa kawaida bali ni shetani na hivyo kuamua kusalimisha maisha yao kwa kujirusha toka ghorofa ya pili.

Mwanaume mmoja alimbeba mtoto wa mwanaume huyo na kujirusha naye hadi chini.

Taarifa ya polisi iliyotolewa jana ilisema kuwa mtoto huyo mchanga amefariki dunia huku watu 10 miongoni mwa waliojirusha wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa hospitalini wakipatiwa matibabu.

Polisi wa jijini Paris wameanzisha uchunguzi wa tukio hilo

No comments:

Post a Comment