KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 1, 2010

Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea Ivory Coast
Wapiga kura nchini Ivory Coast


Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea nchini Ivory Coast, baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa kwanza wa urais kwa zaidi ya miaka kumi.

Uchaguzi huo unanuiwa kumaliza mzozo wa kisiasa uliogawanya taifa hilo ka misingi ya kikabila.

Wawaniaji kumi na wanne waliwania kiti hicho cha urais akiwemo rais wa sasa Laurent Gbagbo, rais wa zamani wa nchi hiyo Henri Konan Bedie na waziri mkuu wa zamani Alassane Ouattara.

Kutakuwepo na duru ya pili ya uchaguzi wa urais ikiwa hakutakuwepo na mshindi wa moja kwa moja.

Wakati huo huo, Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Maifa nchini Ivory Coast amewapongeza raia wa nchi hiyo kwa kudumisha amani wakati wa uchaguzi huo wa urais.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa UN, nchini humo Young Jin Choi amesema Umoja wa Mataifa inatafakari kuwaondoa wanajeshi wake elfu tisa walioko nchini humo.

No comments:

Post a Comment