KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 5, 2010

Serikali ya Rwanda imetangaza kukamatwa kwa katibu mkuu na mweka hazina wa chama cha upinzani cha Unified Democratic ForcesVictoire IngabireViongozi wa chama UDF wakamatwa - Rwanda


Serikali ya Rwanda imetangaza kukamatwa kwa katibu mkuu na mweka hazina wa chama cha upinzani cha Unified Democratic Forces kinachoongozwa na Victoire Ingabire.

Kukamatwa kwa maafisa hao kumejiri siku moja tu baada ya wanachama wa chama hicho, kushutumu hatua ya serikali ya rais Paul Kagame ya kujaribu kuwalazimisha wanachama wa chama hicho cha UDF, kutoa ushahidi dhidi ya kiongozi wao Victoire Ingabire.

Bi Ingabire, alikamatwa na maafisa wa polisi mwezi uliopita na kufunguliwa mashtaka ya kuendesha vitendo vya kigaidi, madai ambayo ameyakanusha.

Katika miezi ya hivi karibuni, serikali ya Rwanda imeshutumiwa na mashirika ya kutetea haki za kibinadam kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza na siasa za upinzani nchini humo

No comments:

Post a Comment