KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 1, 2010

Sensa ya China yaanza leo


Wafanyakazi wa Kichina na Waafrika


Shughuli ya kuhesabu watu au Sensa nchini China, nchi iliyo na idadi kubwa ya watu duniani imeanza.

Serikali ya nchi hiyo inatarajia sensa hiyo itatoa takwimu kamili ya idadi ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini humo. Inakisiwa zaidi ya watu milioni 200 raia wa kigeni wanafanya kazi nchini humo.

Vile vile sensa hiyo inatarajiwa kutoa idadi kamili ya watoto. Mwandishi wa BBC mjini Beijing amesema kutokana na sheria ya nchi hiyo inayopiga marufuku familia kuwa na zaidi ya mtoto mmoja, watu wengi nchini humo hawaiarifu serikali pindi wanapopata mtoto mwingine.

Sensa iliyoendeshwa miaka 10 iliyopita nchini humo, ilibainisha idadi ya watu nchini humo ilikuwa bilioni moja na nukta tatu.

No comments:

Post a Comment