KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 5, 2010

Ndege ya abiria ya nchini Cuba imedondoka katikati ya nchi hiyo na kuua watu wote 68



Ajali ya ndege ya Cuba yauwa 68

Ndege ya abiria ya nchini Cuba imedondoka katikati ya nchi hiyo na kuua watu wote 68 waliokuwa ndani yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Cuba inayosimamia safari za ndege, waokoaji hawakumpata mtu yeyote aliye hai.

Ndege hiyo ya Shirika la Kitaifa Aerocaribbean ilikuwa safarini kutoka mji ulio mashariki wa Santiago de Cuba kwenda mji mkuu Havana.

Miongoni mwa abiria walikuemo watu kutoka nchi za kigeni 28. Wengine 33 na wahudumu saba wote ni raia wa Cuba. Hakuna taarifa yoyote kuhusu kilichosababisha ajali hiyo.

Ndege hiyo iliyoundwa nchini Ufaransa aina ya ATR ilidondoka majira ya magharibi siku ya Alhamisi karibu na mji wa Guasimal katika jimbo la Santi Spiritus. Wengi wa abiria wake wote inaaminika walikuwa ni watalii.

Taarifa ya Mamlaka ya Safari za ndege za abiria imesema kuwa orodha ya wageni waliokuwa kwenye ndege hiyo ni raia tisa kutoka Argentina, saba kutoka Mexico. Raia watatu Wadachi, Wajerumani wawili, Wa Austria wawili, raia mmoja wa Ufaransa, mmoja kutoka Itali, M-Hispania mmoja kutoka Venezuela na Mjapani mmoja.

Ndege hiyo inayofanya safari mbili kila wiki ilianza safari yake huko Port-au-Prince visiwani Haiti na kutua kwa mda mjini Santiago.

Rubani alitowa taarifa ya dharura kabla ya mawasiliano kupotea.

Makundi ya waokoaji pamoja na wakaazi wa hapo walilazimika kutumia Makarandinga kufyeka msitu mkali ili kuweza kufika mahali pa ajali, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Cuba.

Baada ya kufikia mahali pa ajali maiti ziliondolewa ndani ya mabaki ya ndege lakini hakuna aliyepatikana kuwa hai. Mtu mmoja aliyeshuhudia ameelezea mahali pa tukio kama ''Mdwara wa moto katikati ya Kilima''




Haijafahamika kama hali mbaya ya hewa ilichangia kutokea kwa ajali hiyo. Kabla ya hapo onyo la kutokea kwa dharuba lilitolewa katika jimbo la Santiago de Cuba ambako ndege hiyo ilitua na kupaa baadaye.

Kwa wakati huu, Mamlaka ya safari za ndege na wakuu wa huko wanatafakari na kuchunguza maelezo. Tume ya kuchunguza ajali hiyo imeundwa na Mamlaka ya safari za ndege za raia.


Vyombo vya habari vimearifu kuwa hii ndiyo ajali mbaya kuwahi kutokea nchini Cuba tangu Ndege ya Kirusi aina ya Ilyushin -62 ikiwa njiani kuelekea Milan ilipondondoka tareh 3 septemba mwaka 1989 ikiua watu 126 waliokuwa wakisafiri

No comments:

Post a Comment