KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, November 6, 2010

Mkuu wa genge la mihadarati auwawa Mexico




Tony Tormenta
Mmoja wa viongozi wa magenge ya madawa ya kulevya nchini Mexico amepigwa risasi na kuuwawa na vikosi vya usalama karibu na mpaka wa Marekani.

Ezequiel Cardenas, aliyejulikana kwa jina la Tony Tormenta, aliongoza genge liitwalo Gulf kuanzia mwaka wa 2007 baada ya mdogo wake Osiel kukabidhiwa Marekani kwa lengo la kufunguliwa mashtaka.

Wakaazi katika mji wa (Matamoros) ambako Cardenas aliuwawa walitumia Twitter na Youtube kurepoti mapambano ya kutumia silaha yaliyodumu kwa saa kadhaa.

Watu watatu wenye silaha na askari wawili waliuwawa, pamoja na mwandishi wa habari aliyejikuta katikati mwa mapambano hayo makali.

Rais wa Mexico, Felipe Calderon, aliahidi mapambano makali ya kuwasaka viongozi wa magenge ya madawa ya kulevya wakati alipoingia madarakani miaka minne iliyopita

No comments:

Post a Comment