KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 5, 2010

Matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Ivory Coast yamebainisha kuwa hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asili mia 50


Rais anapambana na muungano wa upinzani


Kura kurudiwa tena


Matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Ivory Coast yamebainisha kuwa hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asili mia 50 ya kura na hivyo itahitaji duru ya pili ya kutafuta mshindi na safari hii watashindana wagombea wawili.

Hao watakuwa mshindi wa kwanza na wa pili. Rais wa sasa Laurent Gbagbo aliongoza kwa asili mia 38 ya kura akifuatiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Alassane Ouattara aliyepata asili mia 32 ya kura. Rais wa zamani Henri Konan Bedie alimaliza wa tatu akizoa asili mia 25 ya kura.

Ingawa Rais Gbagbo alishinda duru hiyo, lakini ameshindwa kutimiza kiasi cha kura zinazohitajika huku akikabiliwa na upinzani mkali kutoka ushirika wa vyama vya wagombea katika duru ijayo, inayokisiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba.

Matokeo haya yamewasilishwa kwa Mahakama ya kikatiba kuidhinishwa wakati Umoja wa Mataifa unahitaji kuthibitisha matokeo. Matokeo haya ni ishara ambayo huenda mkongwe wa siasa Henri Konan Bedie amefikia kikomo cha uwezo wake kisiasa.





Mkongwe afika kikomo

Rais huyo wa zamani ametangaza kuwa atapinga matokeo hayo, ambayo msemaji wake ameyataja kama yaliyodhihirisha 'njama ya kuiba matokeo'

Hata hivyo wasimamizi wa Kimataifa wameutaja mchakato mzima kama uliofanyika kwa uwazi na usawa, licha ya kuwepo mapungufu ya mipango.

Na baada ya siku nyingi za wasiwasi na hali ya sintofahamu, Biashara nyingi huenda zikafunguwa milango kuanza shughuli zake mjini Abidjan ingawa duru hii ya pili itakuwa kali.

Ouattara anashirikiana na muungano wa upinzani ulio na mgombea mwenza Bedie na vyama vingine vidogovidogo vilivyomuezesha kushinda asili mia 60 katika duru ya kwanza.

Hata hivyo kuna hofu kama kura zote za Bedie kutoka sehemu ya kati mashariki itaelekea katika kambi ya Bw.Ouattara ambayo inamiliki eneo la kaskazini lenye idadi kubwa ya Waislamu.

Majuma kadhaa yajayo kabla ya duru hiyo ya pili inatazamiwa kuwa majibizano makali na madongo yatarushwa wakati Rais aliyekua madarakani akijitahidi kuzoa kila wapiga kura kutoka kwa muungano wa upinzani

No comments:

Post a Comment