KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Maandamano makubwa kupinga ada Uingereza

Maandamano London



Maelfu ya wanafunzi pamoja na wahadhiri wameandamana eneo la Bunge la Uingereza la Westminster wakipinga kuongezwa ada ya masomo na kupunguzwa mgao wa fedha zinazotolewa kwa vyuo vikuu vya England.



Mawaziri wametangaza mipango ambapo vyuo vikuu vya England vitakuwa na uwezo wa kutoza ada kwa wanafunzi hadi paundi elfu tisa kwa mwaka kuanzia mwaka 2012.

Naibu Waziri Mkuu Nick Clegg amekwaruzana bungeni na naibu kiongozi wa chama cha Labour, Harriet Harman kuhusiana na mipango hiyo ya serikali.

Viongozi hao walikwaruzana wakati wa kikao cha maswali kwa Waziri Mkuu wakati huu David Cameron akiwa ziarani China na Ed Miliband yupo likizo.

Watu walioshuhudia maandamano hayo wameyaeleza ni makubwa kuwahi kufanyika tangu serikali ilipotangaza mipango yake ya kupunguza matumizi mwezi uliopita na sababu kwa nini wanafunzi na wahadhiri wamekasirishwa ni kutokana na ukubwa makato ya vyuo vikuu vya England.

Katika baadhi ya vyuo vikuu huenda wanafunzi wakalipa ada mara tatu ya wanayolipa kwa wakati huu

No comments:

Post a Comment