KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, November 1, 2010

Kura zinahesabiwa nchini TanzaniaWafuasi wa CCM

Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea nchini Tanzania siku moja baada ya uchaguzi mkuu uliokuwa na msisimuko mkubwa kuwahi kushuhudiwa tangu kuanzishwa siasa za vyama vingi nchini humo miaka ya 1990.

Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa siku ya Jumatano.

Rais wa sasa Jakaya Kikwete amesema anatarajia kutetea kiti hicho cha Urais
Wafuasi wa chama cha CUF

Kikwete alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Willibrod Sla ambaye alitumia muda mwingi wakati wa kampeini kupinga ufisadi.

Chama tawala cha Mapinduzi CCM, ambacho kimekuwa madarakani tangu nchi hiyo ilipojinyakulia uhuru, ilikabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama kadhaa vya kisiasa, kufuatia kushuka kwa umaarufu wa serikali kutokana na madai ya ufisadi.

Kura kadhaa za maoni zimeonesha Rais Kikwete huenda akashinda muhula mwingine kuwa Rais wa nchi hiyo.

Hata hivyo kura nyingine ya maoni ilionyesha mpinzani wa Rais Kikwete, Wilbord Slaa wa chama cha CHADEMA alikuwa akiongoza japo kwa kiasi kidogo sana

No comments:

Post a Comment