KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 10, 2010

Kipindupindu chawaua watu 540 Haiti


Kipindupindu chazidi Haiti




Madaktari katika mji mkuu wa Haiti, Port au Prince, wamesema mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umetokea mjini humo ingawa hapajakuwa na thibitisho rasmi.

Zaidi ya watu 540 wamekufa kufuatia maradhi hayo na wengine takriban 8000 wanatibiwa hosipitalini.

Kuna wasiwasi maradhi hayo huenda yakasambaa kwa haraka katika kambi za mji wa Port-au-Prince zinazowasitiri waathiriwa wa tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Januari mwaka huu.

Juhudi za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo zinavurugwa na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga cha Tomas kilichopiga Haiti mwishoni mwa juma

No comments:

Post a Comment