KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, November 8, 2010

Ajeruhiwa nyeti kwa wivu wa mapenzi!


MWANAMKE mmoja [30] jina kapuni anaendelea kujiuguza katika zahanati binafsi baada ya kujeruhiwa sehemu za siri na mumewe kwa kuonekena kuwa alitoka nje ya ndoa.
Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, mume wa mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la Beka alikuwa na wivu wa kupindukia kwa mke wake huyo hali inayomfanya mwanamke huyo kukosa amani kwa mume wake huyo.

Ilidaiwa kuwa siku ya tukio juzi majira ya saa 2 usiku, mwanamke huyo alikuwa akitoka katika sherehe ya kitchenparty ya jirani yao na kumkuta mume wake huyo amefura kwa hasira kutokana na kuhisi huenda mke wake huyo hakutokea kwenye sherehe bali alitumia mbinu ya kumdanganya.

Ilidaiwa kuwa mume huyo alianza kumuhoji mke wake huyo kua ametoka wapi na kumjibu “ ni ile sherehe niliyokuaga ndiyo nimetoka huko” na mume huyo kumjibu kuwa hakutoka huko na kufanya majibizano ya hapa na pale.

Ilidaiwa kuwa muda mfupi baadae , mwanamke huyo akiwa chumbani mume wake huyo alimuamuru amkague sehemu zake nyeti hali iliyofanya mwanamke kustaajabu na kujua mume wake huyo anamtania kama ilivyo mke na mume kutaniana ni kawaida.

Kwa kuwa mume huyo hakuamini kabisa kama mke wke ametoka kwenye sherehe hiyo alianza kufanya ukaguzi kwenye mwili wa dada huyo na mwanaume huyo kumwambia dada huyo amembaini kuwa ametoka kwa bwana wake.

Hivyo kabla hajainuka mume huyo alimjeruhi mke wake huyo na kukwambia hiyo ndio dawa yake na atakoma kufanya tena siku nyingine.

Ilidaiwa kuwa dada huyo alipata maumivu makali sehemu hizo na kumwita mdogo wake usikun huo amsaidie kumpelekea zahanati ya karibu na kumueleza mkasa huo

Nifahamishe ilipowasiliana na chanzo cha habari hii asubuhi hii, kilidai kuwa mwanamke huyo anaendelea vizuri na ataruhusiwa muda wowote kuanza sasa, na kudaiwa hatarudi kwa mumewe huyo na badala yake atakwenda kupumnzika nyumbani kwao maeneo ya Tegeta

No comments:

Post a Comment