KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 26, 2010

Upinzani Bahrain wakosoa uchaguzi



Uchaguzi wa Bahrain

Maafisa wa serikali nchini Bahrain wamekataa shutma za kundi kubwa la upinzani la Washia kuwa mamia ya wapiga kura wake walizuwiliwa kupiga kura katika uchaguzi wa bunge uliofanyika siku ya Jumamosi.

Waziri wa Sheria wa Bahrain, Sheik Khaled bin Ali Al Khalifa, alisema kulikuwa na visa vichache vya ukiukwaji wa taratibu za kupiga kura, lakini kwa ujumla uchaguzi ulikuwa wa haki.

Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa leo.

Wanaharakati kadhaa wa Kishia walitiwa mbaroni wakati wa maandalizi ya uchaguzi, na serikali imeshtumiwa kwa kukwamisha uhuru wa kujieleza.

Washia ndio wengi zaidi nchini Bahrain, lakini watawala wa nchi hiyo ya kifalme ni Waislamu wa madhehebu ya Kisunni.

No comments:

Post a Comment