KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, October 22, 2010

Migomo na maandamano yachacha Ufaransa


Baada ya vurugu kwenye miji mbalimbali ya Ufaransa, vyama vya wafanyakazi vinapanga kuandaa migomo zaidi mnamo tarehe 28 mwezi huu na tarehe 6 Novemba.Wafanyakazi wengi nchini humo walijitokeza mitaani kupinga hatua ya serikali ya kuongeza umri wa kustaafu kwa miaka miwili zaidi.

Kwa sasa umri wa kustaafu kwa wafanyakazi wa umma ni miaka 60.

Wakati wowote, seneti inatazamiwa kupiga kura kuhusu mswada wa kubadilisha umri huo.

Serikali pia inapendekeza kwamba mstaafu ataweza tu kupokea mafao yake kamili baada ya kutimiza miaka 67 na sio 65 kama ilivyo kwa sasa.

Swala hilo limesababisha maandamano katika sehemu mbalimbali nchini Ufaransa ikiwa ni pamoja na mji mkuu Paris na mingine kama vile Lyon, Marseille, Toulouse na Bordeaux.

No comments:

Post a Comment