KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, October 22, 2010

China yakiuka vikwazo vya UM na kuuza silaha Darfur



Makundi ya waasi yamekuwa yakikabiliana na serikali katika eneo la Darfur


Umoja wa Mataifa umedai kwamba China inajaribu kuzuia kuchapishwa kwa ripoti ambayo inaonyesha kuwa nchi hiyo imeendelea kuuza silaha zake katika eneo la Darfur Kusini mwa Sudan licha ya vikwazo vya Umoja huo.

Ripoti hiyo ambayo tayari imewasilishwa inadai kuwa risasi zilizotengenezwa nchini China zimepatikana katika maeneo ya mashambulizi yaliotekelezwa dhidi ya majeshi ya kulinda amani ya Umoja huo.

Hata hivyo haijabainika iwapo silaha hizo ziliuziwa serikali ya Sudan au la. Balozi wa China katika umoja huo Zhao Baogang, amesema ripoti hiyo ina dosari nyingi.

Zaidi ya watu laki tatu wameuawa katika eneo la Darfur katika mapigano kati ya jeshi la Sudan na makundi ya waasi.

No comments:

Post a Comment