KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, September 8, 2010

Vatican yashtumu kuchomwa kwa Quran.Vatican yashtumu kuchomwa kwa Quran.

VATICAN

Mpango wa kanisa hilo la Florida-Marekani kuchoma moto Quran tukufu pia umekosolewa na Makao makuu ya Kikatoliki duniani, Vatican. Katika taarifa yake, Vatican ilisema mpango wa kuzichoma moto nakala za kitabu kitakatifu cha Waislamu ni ouvu na ishara mbaya dhidi ya Waumini wa Kiislamu na kitabu chao kitakatifu. Makao hayo makuu ya Wakatoliki yalisema ingawa mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani Septemba 11 yalikuwa yakuchukiza, huwezi kulipia kwa ishara za ouvu dhidi ya kitabu kitakatifu cha waumini wa jamii fulani. Wakati huo huo kanisa moja dogo hapa Ujerumani liliojitenga na mchungaji Terry Jones mwaka wa 2008, limetangaza kujitenga na mpango huo wa kuzichoma moto nakala za Quran. Stephen Baar, Kiongozi wa jamii ya Wakristo, mjini Cologne, iliyoanzishwa na Jones miaka 80 alisema walijitenga na mchungaji huyo wa Marekani miaka miwili iliopita kwa sababu alikuwa analiongoza kanisa katika njia mbaya.

Mpango huo wa kutaka kuzichoma moto nakala za kitabu hicho kitakatifu pia imekosolewa vikali na ulimwengu wa Kiislamu

No comments:

Post a Comment