KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, September 8, 2010

Tuzo kwa mchoraji vibonzo vya Mtume MuhammadTuzo kwa mchoraji vibonzo vya Mtume Muhammad

BERLIN

Mchoraji vibonzo kutoka Denmark maarufu kwa ile kashfa ya kuchorwa vibonzo vilivyomdhihaki Mtume Muhammad, atapewa tuzo hapa Ujerumani, kesho. Kurt Westergaard, ambaye mwaka wa 2005 alichora vibonzo vilivyoonyesha Mtume Muhammad amevaa bomu katika kilemba chake, atakabidhiwa tuzo hilo la M 100 la uandishi wa habari na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Kamati iliyoandaa tuzo hiyo imemsifu Westergaard kwa ujasiri wake kupigania uhuru wa uandishi na uhuru wa kutoa maoni.

Wakati huohuo, Kiongozi wa baraza kuu la Waislamu nchini Ujerumani Nadem Elyas ameikosoa hatua hiyo ya kumtunza Westergaard.

Vibonzo hivyo vya Westergaard vilivyochapishwa katika gazeti la Denmark, Jylaands Posten, vilizusha hasira kali na maandamano katika Ulimwengu waKiarabu na kiislam.

MWENYEZI MUNGU ALIFICHA SURA ZA MITUME WAKE, ILIBINADAMU WENYE UPUNGUFU WA AKILI KAMA
Westergaard WASIJE WAKAWAKASHIFU WATU BORA WALIOTUMWA KUONGOZA UMMA KATIKA NJIA TAKATIFU. WALA SIJAMBO LAKUSHANGAZA KUONA Westergaard AKIPEWA TUNZO KWASABABU WOTE WATOA TUNZO NI WAPINZANI WA QURAN, UISLAMU NA WAISLAMU DUNIANI, WALA HAWANA TAFAUTI NA WALE WENYE KUWAUWA WAISLAMU NA KUWADHULUMU MALIZAO KATIKA JINA LA UGAIDI. WAISLAMU WAMEZOEA KUPIGWA AU KUSHAMBULIA KILA UPANDE KATIKA JINA LA UGAIDI, UHURU WAKUONGEA NA DEMOKARASIA. HUU SIO USTARABU AMBAO WALE AMBAO SIO WAISLAMU WANAWATENDEA WAISLAMU. MWISHO WA YOTE VITAIBUKA VITA VYA KULIPIZA KISASI NA WAISLAMU WATAONEKANA NI WAKOROFI!

No comments:

Post a Comment