KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 21, 2010

Mtoto wa miaka miwili wa kike wa nchini Marekani akivuta bangi

Mtoto wa miaka miwili wa kike wa nchini Marekani akivuta bangi

Polisi wa nchini Marekani wametoa VIDEO inayomuonyesha mtoto wa kike wa miaka miwili akivuta bangi.
Polisi wa nchini Marekani wametoa video inayomuonyesha mtoto wa kike mwenye umri wa miaka miwili akivuta sigara ambayo imechanganywa bangi.

Polisi wa Cincinnati, Ohio nchini Marekani walitoa video hiyo ambayo mama wa mtoto huyo anayeitwa Jessica Gamble mwenye umri wa miaka 21, anasikika akimfundisha binti yake huyo jinsi ya kuivuta vizuri bangi.

Taasisi inayoshughulikia masuala ya familia ya Ohio, ilipewa video hiyo mwezi uliopita na mtu ambaye alishuhudia tukio hilo lilipotokea mwezi juni mwaka huu.

Mama wa mtoto huyo huenda akatupwa jela miaka 11. Pia mama huyo anakabiliwa na kesi ya madawa ya kulevya na atapandishwa kizimbani baadae mwezi huu

No comments:

Post a Comment