KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, September 1, 2010

Mgahawa wa Nyama za Binadamu Wafunguliwa Ujerumani





Tovuti ya mgahawa utaouza nyama za binadamu Monday, August 30, 2010 12:38 PM
Mgahawa unaouza nyama za binadamu unafunguliwa mjini Berlin nchini Ujerumani mwezi ujao na tayari umeishaanza kusababisha mtafaruku mkubwa nchini humo.
Tovuti ya mgahawa huo utakaofunguliwa mjini Berlin nchini Ujerumani iliwaomba watu wajitolee viungo vya miili yao ili kuwezesha menu za vyakula za mgahawa huo.

Tovuti hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Filme ya mjini Berlin ilisema "Changia kiungo chochote cha mwili wako" pia kampuni hiyo ilisema kuwa inamtafuta daktari atakayeweza kufanya operesheni za kukata nyama za binadamu.

Hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la Der Spiegel, wanasiasa nchini humo wamelaani vikali kufunguliwa kwa mgahawa huo.

Hadi sasa sehemu ambayo mgahawa huo ambao utafunguliwa septemba nane mwaka huu imefanywa siri haijatangazwa.

Mgahawa huo umedai umefunguliwa kufuatiwa kuvutiwa na tamaduni za kabila la Waricaca la nchini Brazili ambalo baadhi ya watu wake hula nyama za binadamu.

Watu watakaotaka kujitolea viungo vya miili yao hutakiwa kujaza fomu za kuelezea afya zao na kama ni mwanamke hutakiwa kusema kama ni mjamzito.

Michael Braun, makamu wa rais wa chama cha Christian Democrats cha mjini Berlin aliliambia gazeti la Bild la nchini humo kuwa amepokea email nyingi sana za watu wanaolalamika kufunguliwa kwa mgahawa huo.

"Nadhani watakuwa wanatania kufungua mgahawa kama huu maana inatia kinyaa", alisema Braun.

No comments:

Post a Comment