KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, September 2, 2010

Kama Siku ya Kufa Haijafika...


Mwanaume mmoja wa nchini Marekani kwa sababu ambazo hazijaeleweka amejirusha toka kwenye paa la jengo la ghorofa 40 lakini bado yuko hai pamoja na kwamba alidondokea juu ya gari lililokuwa limepaki chini.
Mwanaume huyo ambaye polisi walimtaja kwa jina la Thomas Magill, alijirusha toka kwenye paa la jengo la ghorofa 40 lililopo kwenye barabara ya 63 ya jijini New York.

Taarifa zilisema kuwa mwanaume huyo baada ya kujirusha alidondokea kwenye gari aina ya Dodge Charger lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara hiyo.

Alidondokea kwenye kioo cha nyuma cha gari hilo ambacho kilivunjika na Magill alijikuta akiwa kwenye siti ya nyuma ya gari hilo.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa Magill anaendelea vizuri sana ingawa amevunjika miguu yake.

Polisi wanafanya uchunguzi kujua sababu ya mwanaume huyo kujirusha.

Mwaka 2007 mwezi disemba, msafisha vioo kwenye majengo aliyejulikana kwa jina la Alcides Moreno alidondoka toka ghorofa ya 47 wakati akisafisha vioo lakini pia alinusurika maisha yake.

No comments:

Post a Comment