KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, September 1, 2010

Idadi ya raia Kenya yafikia milioni 38





Idadi ya wakazi nchini Kenya imefikia milioni 38.6 (38,610,097), takwimu hizo ni kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2009. Kati ya takwimu hizi idadi ya wanaume kwa wanawake imeonekana sawa jinsia zote zikifikia milioni 19.4 wanawake na milioni 19.2 wanaume.

Akitangaza matokeo ya sensa waziri wa mipango ya taifa, Wycliffe Oparanya, hata hivyo amesema matokeo ya wilaya nane yalibatilishwa kutokana na dosari katika kukusanya idadi ya raia wa maeneo hayo.

Wilaya ambazo idadi ya raia haikutolewa ni zile za Kaskazini mwa Kenya ikiwa ni pamoja na Lagdera, Wajir Mashariki, Mandera Kati, Mandera Mashariki, Mandera Magharibi, Turkana Kati na Turkana Kusini.

Idadi ya raia wa Kenya imefika milioni 38, uwingi wa wanawake na wanaume hautofautiani sana.

Bw Oparanya amesema dosari hizo zilipatikana baada ya idadi ya raia kuonekana kuwa juu kuliko nakili za watoto wanaozaliwa na ripoti ya vifo.
Mchanganuo

Matokeo ya sensa hiyo yaliganywa kwa misingi ya maeneo, jinsia, umri, dini, na kabila.

Kabila la kikuyu ndilo lenye raia wengi zaidi nchini Kenya wakiwa milioni 6.62, Luhya wanafuata Milioni 5.33, Kalenjin milioni 4.96, Luo Milioni 4.04 na Kamba wakifunga kabila tano kubwa kwa raia milioni 3.89.

Wengine ni pamoja na Kenyan Somali (2.38 milioni), Kisii (2.21 milioni), Mijikenda (1.96 milioni), Meru (1.65 milioni), Turkana (0.99 milioni), Maasai (0.84 milioni), Teso (0.33 milioni) na Embu (0.32 milioni).

Katika upande wa mseto wa dini ya imani ya Protestanti ina wafuasi wengi zaidi nchini Kenya wakiwa na waumini milioni 18.3, kanisa Katoliki linafuata likiwa na wafuasi milioni 9,010,684 huku imani nyingine za kikiristo zikiwa na waumini 4,559,584.

Takwimu zinaonyesha Kenya ina waislamu 4,304,798 huku wahindi ni 53,393.
Marekebisho

Sensa ya mwisho nchini Kenya ilifanyika mwaka 1999 ambapo idadi ya raia ilikiwa milioni 28.7. Kufikia sasa Wakenya wameongezeka kwa watu milioni 10 katika muongo mmoja.

Wycliffe Oparanya, Waziri wa mipango ya kitaifa amesema matokeo ya sensa yatasaidia serikali katika usambazaji wa rasilimali za taifa.

Vile vile Waziri Oparanya alisema kwa mara ya kwanza wizara yake itakuwa ikitathmini idadi ya ukuaji wa raia katika kipindi cha kila baada ya miaka mitano.Pia matokeo yatahusisha idadi ya vijana na wazee.


Katika maeneo ya majimbo mapya kama yalivyonakiliwa kwenye katiba mpya, jimbo la Nairobi linaongoza kwa idadi ya watu milioni 3.1 inafuatwa na kakamega, Bungoma, Kiambu, Nakuru na Meru. Majimbo mengine yenye zaidi ya watu milioni moja ni pamoja na Kisii, Kilifi, Machakos na Mandera.

Kwa upande miko, Rift Valley ina watu milioni 10.1, Mkoa wa Mashariki milioni 5.6, Nyanza milioni 5.4, Kati milioni 4.4 na Magharibi Milioni 4.3. Mkoa wa Pwani una watu milioni 3.3, Nairobi milioni 3.1 na Kaskazini Mashariki ikiwa na watu milioni 2.3.

No comments:

Post a Comment