KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 2, 2010

Dawa za serikali huibiwa barani Afrika


Matokeo ya utafiti umethibitisha kuwa dawa za kutibu ugonjwa wa Malaria, zinazotolewa kwa nchi kadhaa barani Afrika huibiwa na kisha kuuzwa katika hospitali na duka za kuuza dawa za kibinafsi.

kwenye ripoti iliyochapishwa na jarida moja la matibabu, watafiti kutoka Marekani na Uingereza walinunua dawa kutoka miji kumi na moja barani afrika na waligundua kuwa moja kati ya ishirini ilikuwa mali ya zahati na hospitali za serikali.

Wataalamu wengine wamethibitisha kuwa matokea ya utafiti huo ni ya kweli. Zaidi ya watu milioni moja hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa malaria barani afrika.

No comments:

Post a Comment