KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, August 26, 2010

Watoto wafa katika ajali Afrika Kusini

Watu wasipungua wanane wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa baada ya basi la wanafunzi kugongana na treni nchini Afrika Kusini.

Ajali hiyo imetokea katika kivuko cha reli karibu na mji wa Cape Town, ambapo dereva alivuka geti la reli lililofungwa, wamekaririwa watu walioshuhudia tukio hilo.

Msemaji wa polisi amesema geti la reli lilikuwa limefungwa wakati ajali hiyo ikitokea.
Kujeruhiwa vibaya

Dereva wa basi ameripotiwa kujeruhiwa vibaya.

Polisi wamesema uchunguzi unaendelea na mashitaka huenda yakafunguliwa dhidi ya dereva.

"Kivuko hicho kina alama za barabarani zinazotoa onyo, na hata taa ambazo zimethibitika kuwa zilikuwa zikifanya kazi sawasawa" imesema taarifa ya shirika la reli.

Ndugu na jamaa wanaoomboleza wamekusanyika katika eneo la tukio.

Hauna mtu aliyeumia katika treni

No comments:

Post a Comment