KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 13, 2010

Ukisikia Ajali Haina Kinga ....


Ajali hii ya kutisha ilitokea nchini Afrika Kusini ambapo dereva wa gari aina ya toyota pickup ambayo ilikuwa imejaza watu wengi nyuma, alipoteza mwelekeo na kupelekea gari ipinduke huku ikiwamwaga hini na kuwasaga watu waliokuwemo kwa gari hiyo.
Katika ajali hii ya kusikitisha, watu wanne walifariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa vibaya sana.

Ajali hii ilitokea nchini Afrika Kusini mwezi wa nne mwaka huu lakini video yake imetolewa hivi karibuni ili watu wajifunze usalama barabarani.

Video ya tukio hili ilichukuliwa na mwanaume mmoja ambaye wakati huo alikuwa akichukua video ya nyumba anayoijenga pembeni ya barabara.

Alifanikiwa kulinasa tukio zima la ajali hii kuanzia wakati dereva aliposhindwa kuukontroo usukani na kuanza kuyumbayumba kabla ya kupinduka na kuwamwaga chini watu saba waliojazana nyuma ya gari hiyo.

No comments:

Post a Comment