KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 17, 2010

Uganda: Jeshi lakanusha madai ya dhuluma Karamoja


Mbunge mmoja nchini Uganda ambaye pia ni mtetezi wa haki za binadamu, Francis Adamson Kiyonga, amewashutumu wanajeshi kwa kuwatesa na kuwauwa raia katika eneo la Karamoja, kama sehemu ya kuwapokonya silaha.

Bw.Kiyonga anadai kikosi cha jeshi la UPDF kilichopiga kambi katika eneo la Tapach, kimekuwa kikiwauwa watu na pia kutumia njia za kikatili kuwalazimisha wakaazi wa eneo hilo kukiri kuwa wanamiliki silaha.

Kikosi hicho kinachoendesha operesheni ya kuwapokonya silaha raia katika eneo hilo, kinaongozwa na mwana wa kiume wa rais Yoweri Museveni, Keinerugaba Muhoonzi.

Jitihada za serikali ya Uganda kurejesha usalama katika eneo hilo hazijafanikiwa, huku operesheni hiyo ikikumbwa na madai ya kuwatesa raia wasiokuwa na hatia.

Msemaji wa jeshi la Uganda, Felix Kulaigye amekanusha madai hayo na kujitetea kwa kusema kuwa ''mtu mmoja au wawili wakihusika na kuwanyanyasa watu, haimanishi kuwa kikosi kizima kimekuwa kikitenda uhalifu''.

Amearifu kuwa wanajeshi watatu wanazuiliwa kwa madai ya kuwanyanyasa raia.

No comments:

Post a Comment