KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, August 2, 2010

Shughuli ya uokoaji yaendelea Pakistan

Mafuriko Pakistan


Maeneo mengi ya Pakistan ya kaskazini magharibi bado yako chini ya maji yaliyosababishwa na mafuriko licha ya kuwa hakuna mvua inayonyesha.

Takriban watu milioni moja na nusu wanakadiriwa kuathirika, wengi wao hawana lolote wala pa kwenda wakisubiri msaada kuwafikia.

Maji masafi yaliyokuwepo yamechafuka na kusababisha hofu ya kueneza maradhi.

Jeshi la Pakistan linasema limejitolea kupeleka askari 30,000 kusaidia kusambaza msaada, lakini juhudi za kuwafikisha waathirika katika maeneo salama inakwenda polepole.

Miongoni mwa wanaohitaji msaada wapo walio katika hali mbaya ya afya wakihitaji kuokolewa kwa wakati.

Takriban watu 1,100 wamefariki na jamii nzima kuteketea katika mafuriko mabaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 80, ikitarajiwa kuwa hadi watu milioni moja na nusu watahitaji msaada.

Kuna hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya kipindupindu miongoni mwa watu wasio na mahali pa kulala. Vile vile chakula na maji vimepungua.

Jeshi ambalo linadai kuwa limeokoa watu 28,000 katika siku chache zilizopita, linatabiri kuwa shughuli ya kusaka na kuokoa wengine itachukua hadi siku kumi.

Halikadhalika jeshi limesema ukarabati wa maeneo yaliyokumbwa na janga hili utachukua hadi miezi sita au zaidi.


Katika eneo moja la kaskazini magharibi, kuna sehemu ya ukubwa wa kilomita 70 ambalo ni marufuku kuingia kukiwa na madaraja 29 yaliyoharibiwa. Huko kuna watu wanaishi katika maeneo yaliyogeuka visiwa.

Baadhi ya watu waliookolewa wamelalamika kuwa juhudi za serikali hazikufanywa kwa kasi inayohitajika katika hali hii.

Wakuu wa serikali mjini Islamabad wanasema kuwa wakati watakapoweza kufika katika maeneo yaliyoathirika ndipo picha halisi itakapobainika.

No comments:

Post a Comment