KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, August 21, 2010

Palestina na Israel kukutana ana kwa ana
Hillary Clinton na Mitchell
Viongozi wa Palestina na Israel wamekubali mwaliko wa Marekani wa kuwataka kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja mwezi ujao.

Pande zote mbili zilisema wana wajibika kufanya mazungumzo kamili ya dhati.

Mark Regev, msemaji wa Waziri Mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu, alisema majadiliano yatakuwa magumu, lakini muafaka wa kihistoria unaweza kufikiwa.

Mkuu wa upatanishi wa Wapalestina, Saeb Erekat, alisema anatarajia kuwa pande zote mbili zitakuwa washirika wa kweli katika mpango wa amani.

Clinton aonyesha matumaini

Akitangaza mkutano huo, ambapo Rais Obama atakuwa mwenyeji mjini Washington, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alisema anatumai kuwa muafaka thabiti wa amani unaweza kufikiwa kwa muda wa mwaka mmoja juu ya masuala muhimu ya mwisho.

Miongoni mwa hayo ni hadhi ya kisiasa ya mji wa Jerusalem, mipaka ya taifa la Wapalestina na haki ya kurejea kwa Wapalestina ambao walipoteza nyumba zao baada ya kuundwa ka taifa la Israel.

Mjumbe maalum wa Marekani wa Mashariki ya Kati, George Mitchell, alisema uvumilivu utahitajika, kwa sababu tofauti zote hazitopatiwa ufumbuzi kwa haraka.

Kundi la wanamgambo la Kipalestina, Hamas, linalodhibiti ukanda wa Gaza, ambalo halitoshiriki majadiliano hayo, lilisema halitotambua matokeo ya mazungumzo hayo

No comments:

Post a Comment