KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 24, 2010

Mwizi Auliwa Kwa Kuchomwa Moto Kichwa na Tumbo Lake


WANANCHI wenye hasira alfajiri ya kuamkia jana walipambana na kundi la wezi katika barabara ya Kawawa palipo na pori la magomeni na Mkwajuni na kufanikiwa kumkamata mwizi mmoja ambaye walimuua baada ya kumchoma moto kichwa chake na tumbo lake
Tukio hilo la aina yake liligusa hisia za wakazi wa Magomeni na Mkwajuni ambapo inadaiwa wahalifu hao walikua kundi la watu sita ambao walimvamia mwendesha pikipiki aliyekua akikokota pikipiki yake majira ya alfajiri.

Wezi hao walimpora mwanaume huyo pikipiki yake na kisha kumkatakata na mapanga na kumtelekeza akiwa amepoteza fahamu.

Hata hivyo kwa hali hisiyo ya kawaida wasamaria wema waliokuwa ndani ya daladala pamoja na wananchi wa jirani wakiwemo vijana waliokuwa wakifanya mazoezi karibu na eneo hilo na waumini waliokuwa wakitoka msikitini muda huo waliamua kupambana na kundi hilo ambapo walikimbia ndani ya msitu huo na kupotelea ng’ambo ya pili.

Wananachi waliwakimbiza wezi hao na kufanikiwa kumtia mkononi mwizi mmoja ambaye walimshushia kipigo cha nguvu na kumng’oa meno kwa kutumia kwa koleo huku wengine wakimkatakata viganja na kuvitenganisha tenganisha.

“Jamani tumeshachoka kuleana sasa ni kuonyesha vitendo tunafanya tunachojua sisi" alisikika mzee mmoja ambaye inadaiwa anafahamiana na mhanga aliyeporwa pikipiki.

Wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigo mwizi huyo, walipokea taarifa kuwa mwanaume aliyeporwa pikipiki amefariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali.

Wananchi hao wenye hasira waliamua kumaliza hasira zao kwa kumchoma moto mwizi huyo.

Inadaiwa kuwa wananchi walimwagia mafuta mwizi huyo sehemu za kichwani na tumboni na kisha walimzungushia mifuko ya pastiki na majani. Moto huo uliweza kumuunguza eneo zima la juu mpaka kupelekea utumbo wake kupasuka ndipo wananchi walipoondoka na kuiacha maiti yake katikati ya barabara.

Baadhi ya wananchi waliongea na Nifahamishe juu ya tukio hilo walidai kuwa wameishachoka na vitendo vinavyofanywa na wahalifu hao kwani walishalalamika muda mrefu juu ya kuondolewa kwa msitu huo.

“Tunamtaka Mkuu wa Wilaya atuambie ukweli kama huu msitu wameupanda kupoteza watu ama wameupanda kwa lengo gani!!.. maana hauna manufaa yoyote kwa wananchi kila siku tunashuhudia uhalifu" alisema Zainabu mkazi wa Kinondoni.

Kwa upande wake Shahibu Hussein ambaye alishuhudia tukio hilo alidai kuwa ndani ya miezi miwili wameishakufa watu watatu, aidha inadaiwa tokea kushamiri kwa msitu huo tayari zilishaokotwa maiti nne zikiwa zimeharibiwa vibaya na wahalifu.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Peter Kalinga alisema kuwa hayupo ofisini ila atalishughulikia kwa kukusanya taarifa kwa watendaji wake na kulitolea ufumbuzi swala hilo .

“Nipo katika kikao, ngoja nilifuatilie nitakupa majibu’ alisema Kalinga kwa njia ya simu.

No comments:

Post a Comment