KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, August 24, 2010

Mtoto wa Miezi 8 Afariki Baada ya Kunyeshwa Vodka


Mtoto wa miezi minane wa nchini Ukraine amefariki dunia baada ya kunyeshwa pombe kali aina ya Vodka.
Mtoto huyo wa miezi minane alifariki katika mji wa Khmelnitsky nchini Ukraine baada ya kupewa pombe kali aina ya Vodka na babu yake.

Taarifa za vyombo vya habari nchini humo zilisema kuwa babu wa mtoto huyo ili kumliwaza mjukuu wake aliamua kumpa pombe kali aina ya Vodka. Muda mfupi baadae mtoto huyo alifariki dunia.

Taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ilisema kuwa uchunguzi wa maiti ya mtoto huyo ulionyesha kuwepo kwa kiasi cha pombe kwenye damu yake ambacho kingeweza kumfanya kumfanya mtu mzima alewe.

Babu wa mtoto huyo ambaye ana umri wa miaka 50 anashikiliwa na polisi baada ya kukiri kumnywesha Vodka mjukuu wake na kupelekea kifo chake

No comments:

Post a Comment