KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, August 30, 2010

Mapigano makali yaendelea mjini Mogadishu


Wapiganaji wa Al shabaab

Wapiganaji wa Al shabaab

Mapigano makali yanaendelea kwa siku ya 7 mfululizo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu kati ya wapiganaji wa Kiislamu na wanajeshi wa serikali ya Mpito nchini humo.

Hapo jana wapiganaji wa kundi la Al Shabaab, walikabiliana vikali na wanajeshi wa serikali na wale wa muungano wa afrika wa kutunza amani.

Zaidi ya watu 100 wameuawa na wengine 250 kujeruhiwa wiki moja tangu kundi hilo la Al shabaab kuanzisha mashambulio makali dhidi ya wanajeshi wa serikali na vikosi vya kigeni.

No comments:

Post a Comment