KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, August 13, 2010

Man City kumsajili Milner

Manchester City leo imeelezea matumaini ya kufanikiwa kumsajili James Milner na Mario Balotelli katika kipindi cha siku chache zijazo.
Milner na Balotelli
Man City yasema ina uhakika kumpata Milner na Balotelli

Habari hizo ni kulingana na meneja wa Man City Roberto Mancini.

Mancini alisema mchezaji wa Inter Milan, Balotelli, huenda akawa amejiunga na Man City kabla ya kumalizika siku ya Ijumaa.
Mchezaji wa Aston Villa, Milner, naye anatazamiwa kuwa mchezaji wa Man City katika kipindi cha "siku mbili au tatu hivi" kulingana na Mancini.
Ireland na Milner

Ireland kuelekea Villa na Milner kujiunga na Man City

Inadhaniwa kwamba Milner, kiungo cha kati cha timu ya taifa ya England,
amechelewa kujiunga na Man City, kutokana na mchezaji Stephen Ireland, kutaka kulipwa pauni milioni mbili, kabla ya kuondoka Man City.
City wameahidi kuilipa Aston Villa pauni milioni 18 ili kumpata Milner, mwenye umri wa miaka 24, huku wakikubaliana Ireland naye ajiunge na Aston Villa.

Lakini Ireland anasisitiza alipwe pauni milioni mbili, ili kuondoka City, kiwango ambacho Man City haitaki kulipa.No comments:

Post a Comment