KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 31, 2010

Hali Hii Isifike Bongo.



Hali ya joto kali inawatesa watu nchini Sudan kiasi cha kwamba watu wanalazimika kuingia ndani ya mafriji makubwa ya viwandani ili kujipoozesha, watu watatu wamefariki dunia jana baada ya kushindwa kutoka ndani ya friji waliloingia.
Joto kali nchini Sudan limepelekea kuibuka kwa biashara ambayo huenda ipo nchini Sudan pekee.

Kutokana na joto kali nchini humo, kumeibuka biashara ya kujipumzisha kwenye mafriji makubwa ya viwandani.

Watu wanalipa paundi tano za Sudan( Takribani Tsh. 2500) kwa kila lisaa limoja wanalotumia ndani ya mafriji ili kuipoozesha miili yao.

Taarifa toka mji wa Port Sudan zinasema kuwa wanaume watatu walikutwa wamefariki ndani ya friji kubwa kama yale yanayotumika viwandani.

Taarifa zinasema kuwa wanaume hao baada ya kulipa paundi tano za Sudan waliingia ndani ya friji kuipoozesha miili yao baada ya kupigwa na joto kali.

Taarifa zaidi zinasema kuwa wanaume hao walifariki baada ya mlango wa friji walilokuwemo kujifunga na wao kushindwa kuufungua mlango huo kwa ndani.

Katika mwezi huu wa nane ambao kawaida huwa ni mwezi wenye joto kali kuliko miezi yote nchini Sudan, watu 13 walikumbwa na shambulio la moyo wakiwa ndani ya mafriji kama hayo

No comments:

Post a Comment