KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 17, 2010

Anusurika kifo baada ya kukwapua


KIJANA mmoja jina halikuweza kupatikana mwara moja, alinusurika kuuawa na watu wenye hasira kali baada ya kumpora mwanamke akiwa ndani ya gari katika maeneo ya barabara ya Kawawa, Ilala Karume jijini Dar es Salaam.
Kijana huyo alikuwa akiendesha shughuli zake za uporaji katika eneo la makaburi ya Ilala kwa kuvizia magari yakisimama maeneo hayo na kupora na kutoweka.

Kijana huyo jana alikiona cha moto baada ya kumpora mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari kisha kukimbia na raia wema wakamkimbiza na kumpata kisha wananchi hao wakajichukulia sheria mikononi mwao kwa kuanza kumpiga.

Hivyo kijana huyo aliweza kupora handbag ambayo ndani yake ilidaiwa kuwa na simu, pesa taslimu, na hati mbalimbali.

Kijana huyo alinusurika kifo baada ya askari wa kituo cha polisi cha Karume kumuokoa kijana huyo huku akiwa hoi akitapakaa damu mwili mzima na hali yake ikionekana hairidhishi.

Uporaji wa aina hiyo umezoeleka maeneo ya Tandale hasa maeneo ya Tandale kwa Tumbo, Mtogole, Popobawa hadi darajani vijana hao wamekuwa wakiranda pembezoni mwa barabara na kukwapua vitu mbalimbali vya thamani kutoka ndani ya mabasi ya abiria.

Waathirika wa uporaji huo hasa ni wanawake ambao mara nyingi hukwapuliwa hereni kutoka masikioni, pete, hadnbag na hata simu wakati unafanya mazungumzo huikwapua na kutoweka nao.

No comments:

Post a Comment